Mambo 10 ambayo kijana hutakiwi kuyafanya
💝 (1). Kuchagua Kazi. Ni vigumu kupata Kazi ukiwa nje ya Kazi. Fanya Kazi uliyoipata upate Kazi unayoitaka. (2). Kuchagua sehemu ya kuishi /kufanyia Kazi. Maisha ni safari ndefu, maisha ni popote, si lazima kukaa mjini. Hauwezi kujua ni sehemu gan iliyobeba mafanikio yako. Chagua sehemu yenye FURSA na si yenye MAGHOROFA. (3). Kuishi bila kuwa na malengo. Maisha si bahati mbaya au nzuri. Maisha ni mipango, Maisha yanaongozwa na malengo. Vile ulivyo leo ni matokeo ya jinsi ulivyopanga jana, na vile unavyoishi leo ndivyo kesho yako itakavyokuwa. PANGA KESHO YAKO SASA. (4). Maisha Ya kuiga. Maisha yako si ya mwenzako, na ya maisha ya mwenzako si ya kwako. Si kila ukionacho ni lazima ufanye, chagua kipi cha kufanya na kipi cha kuacha. Kupitwa na jambo wakat mwingine sio USHAMBA bali ni BUSARA. (5). Kuishi juu ya kipato chako. Ishi kulingana na vile ulivyonavyo na si usivyonavyo. Kuwa na Busara katika MATUMIZI uepukane na MADENI yasiyo na ULAZIMA. RIDHIKA NA VILE ULIVYONAVYO. (6).Kuish...