Mambo 10 ambayo kijana hutakiwi kuyafanya

 💝


(1). Kuchagua Kazi.
Ni vigumu kupata Kazi ukiwa nje ya Kazi. Fanya Kazi uliyoipata upate Kazi unayoitaka.

(2). Kuchagua sehemu ya kuishi /kufanyia Kazi.
Maisha ni safari ndefu, maisha ni popote, si lazima kukaa mjini. Hauwezi kujua ni sehemu gan iliyobeba mafanikio yako. Chagua sehemu yenye FURSA na si yenye MAGHOROFA.

(3). Kuishi bila kuwa na malengo.
Maisha si bahati mbaya au nzuri. Maisha ni mipango, Maisha yanaongozwa na malengo. Vile ulivyo leo ni matokeo ya jinsi ulivyopanga jana, na vile unavyoishi leo ndivyo kesho yako itakavyokuwa. PANGA KESHO YAKO SASA.

(4). Maisha Ya kuiga.
Maisha yako si ya mwenzako, na ya maisha ya mwenzako si ya kwako. Si kila ukionacho ni lazima ufanye, chagua kipi cha kufanya na kipi cha kuacha. Kupitwa na jambo wakat mwingine sio USHAMBA bali ni BUSARA.

(5). Kuishi juu ya kipato chako.
Ishi kulingana na vile ulivyonavyo na si usivyonavyo. Kuwa na Busara katika MATUMIZI uepukane na MADENI yasiyo na ULAZIMA. RIDHIKA NA VILE ULIVYONAVYO.

(6).Kuishi bila AKIBA.
kuweka akiba ni TABIA sio kiwango kikubwa cha Pesa. Jenga tabia ya kujiwekea akiba. Haujui ni kipi kitakupata muda USIOTEGEMEA.

(7). Kuishi kwa kutegemea MSHAHARA.
Mshahara haujawahi kutosha na hautatosha kama ukishindwa kuishi chini ya kipato chako na kuwa na njia mbadala za kuinua kipato chako. JARIBU NJIA ZINGINE MBALI NA MSHAHARA.

(8).Kushindwa Kupangilia MATUMIZI ya Pesa.
Maamuzi yako ya pesa ndiyo yatakayoamua hali yako ya kiuchumi baadaye. Ni muhimu kujua kipi cha kununua, kwa wakati gani na kwa sababu gani. Jifunze kutofautisha kati ya dhima mfano: gari ya kutembelea na kitegauchumi mfano:nyumba au kiwanja. TUMIA PESA YAKO KUNUNUA KITEGAUCHUMI KULIKO DHIMA.

(9).Kushindwa kutumia MUDA wako VIZURI.
Changamoto kubwa inayotukabili vijana ni kushindwa kujua namna ya kutumia vizuri muda.
Tumia muda wako mwingi kujiendeleza ufahamu wako kwa kujisomea, kupanga malengo yako ya maisha, kujiuliza ni wapi ulikosea na nini ufanye ili urekebishe hayo makosa na muda mchache ufanye wa mapumziko na kufanya vitu vya kufurahisha akili yako kama kuangalia movie, mpira, kuingia kwenye mitandao ya kijamii Facebook, watsap n. k. Kumbuka muda ni rasilimali isiyoweza kurudishwa pindi unapopotea.

(10).Kuoa bila ya kujipanga kimaisha.
Hii inawahusu wanaume, swala la kuoa ni pana sana na kila mtu ana vigezo vyake na mtazamo wake kufanikisha jambo hilo. Ila jambo la msingi ni hili, jiandae kwanza kiuchumi kabla hujaingiza majukumu mengine, unapooa ujue umekubali kusaidia upande wa mwanamke, upande wa familia yenu bila kusahau familia yako binafsi. Hata kama maisha ni kusaidiana na huyo utakayemuoa ila nafas yako kama mwanaume ITABAKI pale Pale.
Hatua 7 za kukabiliana na nyakati ngumu maishani
1.KUBALIANA NA HALI HALISI
Pindi unapokuwa unakabiliana na wakati mgumu maishani mwako, usikimbilie kukata tamaa, hatua ya kwanza kufanya ni kukubaliana na ukweli wa hali yenyewe ilivyokupata.
Kamwe hiki si kipindi cha kulaumu, hata kama wewe ndiyo chanzo cha tatizo hilo, bado hupaswi kujilaumu kwa kile ulichokifanya. Lakini pia usilipe nafasi kubwa tatizo hilo katika akili yako, kwani kufanya hivyo ni kuzidi kulikuza. Kuwa mtulivu tafuta njia ya kulitatua.
2.USIMWELEZE KILA MTU
Watu wengi hukosa uvumilivu pindi wanapokuwa katika nyakati ngumu maishani na kujikuta wakigeuka waropokaji kwa kila mtu wakidhani kwa kufanya hivyo kutasaidia kutatua matatizo yao, jambo ambalo si kweli.
Pamoja na ukweli kwamba matatizo huhitaji msaada wa kimawazo kutoka kwa watu wengine lakini si kwa kila mmoja unayekutana naye au kumuona. Jaribu kuwafuata baadhi ya watu ambao unaamini kuwa wanaweza kuleta suluhu, ukimweleza kila mtu ni rahisi kupata ushauri wa kukuvunja moyo.
3.USIKAE BILA KUJISHUGHULISHA
Epuka sana kukaa bila kujishughulisha kiakili na kimwili kila wakati ili kuitokomeza hali ya huzuni na maumivu unayokabiliana nayo kwa kipindi hiki.
Pendelea kufanya baadhi ya vitu vinavyoweza kukuletea faraja na furaha, mfano labda kujisomea baadhi ya maandiko yatakayokupa mwanga, fanya mazoezi, angalia hata mechi mbalimbali za mpira pamoja na mambo ambayo unaamini ukiyafanya utapata mwelekeo mpya kimtazamo.
4.EPUKA MFADHAIKO
Hupaswi kukaa peke yako muda mrefu, kwani kwa kufanya hivi unakaribisha mfadhaiko akilini mwako kutoka na ugumu wa kimaisha unaokutana nao. Changamana na makundi ya watu wenye furaha ili wakusaidie kuponya huzuni yako.
5.JIAMINI, TUMIA UWEZO WAKO WOTE
Ndani yako kuna uwezo mkubwa sana ambao ukiutumia kikamilifu, unaweza kutatua baadhi ya mambo bila hata ya kuhitaji msaada kwa mtu mwingine. Unapaswa kujiamini. Usiwe na mashaka na uwezo ulionao ndani yako. Tambua maisha ni safari na dereva wake ni wewe.
6.USIKATE TAMAA
Katika maisha watu wengi hukwama kutatua changamoto zao si kwa sababu hawana uwezo la, ila ni ile hali ya kukata tamaa mapema inapowakumba.Kwenye maisha hakuna kukata tamaa, hata kama hali ni ngumu kiasi gani usikubali kushindwa, endelea kupambana hadi tone la mwisho la jasho lako litakapoanguka ardhini, ari hii ni silaha kubwa sana ya kufanikiwa katika kupata furaha unayoitafuta.
7.PAZA SAUTI YA USHINDI
Watu wengi wanapokuwa kwenye hali ngumu za kimaisha hudhani kuwa watakuwa hivyo milele. Maisha yanapita, kila kwenye shida paza sauti moyoni mwako, kila mara jitangazie kuwa HILI NALO LITAPITA.

MUHIMU : UJANA NI KIPINDI AMBACHO NAKIFANANISHA NA KAMA SHAMBA LENYE UDONGO MZURI LINALOPOKEA KILA AINA YA MBEGU.. SASA ITATEGEMEA UNAPANDA NINI..! JIPANGE KWANZA.

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

VITA VYA DUNIA HISTORIA YA MBAVU MOYA

Unakaribishwa we mgeni wa ulimwengu wa mtandao

Zijuwe sharti za google adsense