Articles

Affichage des articles du mars, 2018

KANUNI 30 KWA WANAWAKE NDANI YA NDOA*

1). Usinyanyue sauti mbele ya mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima. 2). Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako. 3). Usitumie mhemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha. 4). Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka. 5). Usiwatendee vibaya marafiki wa mumeo kwa sababu huwapendi, mtu anayetakiwa kuwa wa kwanza kujitenga nao ni mumeo. 6). Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako. 7). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mwenyewe. 8). Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na kumshajiisha. 9). Usiwe mke mwenye m

UBORA WA KUISHI NA WATU VYEMA

SIKU moja, kijana mmoja akitokea mihangaikoni, alimwona Mama fulani akiwa amesimama nje ya gari yake, pembezoni mwa barabara. Licha ya giza la usiku, kijana aliweza kugundua Mama yule yuko taabuni akitarajia msaada. Kijana alijiweka tayari kutoa msaada na kumsogelea. Pamoja na bashasha usoni mwa kijana, bibi alijawa na hofu juu ya usalam wake. Kwa takribani saa kadhaa alizokwama mahala pale, hakuna aliyesimama kumsaidia. Hivyo, kwa ujio wa kijana yule, mwenye haiba ya njaa na mchoko wa umasikini, bibi alibaki njia panda. Hakujua endapo atapata msaada au madhila. Baada ya salaam, kijana alijitambulisha: "Ninaitwa Rama Mgonja. Nimekuja kukusaidia tu, ondoa hofu." Tatizo la gari halikuwa kubwa - tairi lilikuwa na pancha - japo kwa mama wa makamo kama yale, lilikuwa ni tatizo kubwa. Bila kurefusha muda, Rama akaingia uvunguni mwa gari ili kuipachika uzuri jeki. Ndani ya dakika chache tu, tayari akalitoa tairi bovu na kufunga zima. Zaidi ya kuchafuka kidogo tu mikono na nguo za

TUMSIFU YESU KRISTO*

Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.* *Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.* *Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la