Jinsi ngono inavyo angamiza maisha ya vijana
Zamani soko la ngono lilikuwa likisimamiwa na wazee na jamii yote kwa ujumla . Ilikuwa vigumu sana kwa vijana kujiingiza kwenye mahusiano kabla ya ndoa kwa sababu jamii iliweka mipaka kwenye mahusiano . Mipaka ya mahusiano mara nyingi iliendana na mahitajio ya kiimani, hii ilipelekea kukubalika kwa utaratibu kwamba ili kijana kushiriki ngono ilimlazimu kuingia kwenye ndoa. Inawezekana ndio sababu likaitwa tendo la ndoa , yaani linalofanyika ndani ya ndoa pekee. Katika dunia ya leo, soko la ngono limekosa msimamizi halisi . Mamlaka za kidunia zimeingilia kati kufuatia mahitajio ya wanawake kutaka usawa kwenye ngono (sexual revolution) na kuweka uwanja sawa wa biashara hii. Matokeo yake wazee hawana tena uwezo wa kusimamia soko hili ili mnunuzi na muuzaji wawe wamekidhi vigezo vya kiasili, badala yake kila mtu anaingia sokoni vile atakavyo. Hatari kubwa kwa vijana Kwa kuwa leo hii hakuna anayesimamia soko la ngono, jamii imekubali kwamba hakuna tena um...
Commentaires