Jinsi ngono inavyo angamiza maisha ya vijana
Zamani soko la ngono lilikuwa likisimamiwa na wazee na jamii yote kwa ujumla. Ilikuwa vigumu sana kwa vijana kujiingiza kwenye mahusiano kabla ya ndoa kwa sababu jamii iliweka mipaka kwenye mahusiano. Mipaka ya mahusiano mara nyingi iliendana na mahitajio ya kiimani, hii ilipelekea kukubalika kwa utaratibu kwamba ili kijana kushiriki ngono ilimlazimu kuingia kwenye ndoa. Inawezekana ndio sababu likaitwa tendo la ndoa, yaani linalofanyika ndani ya ndoa pekee.
Katika dunia ya leo, soko la ngono limekosa msimamizi halisi. Mamlaka za kidunia zimeingilia kati kufuatia mahitajio ya wanawake kutaka usawa kwenye ngono (sexual revolution) na kuweka uwanja sawa wa biashara hii. Matokeo yake wazee hawana tena uwezo wa kusimamia soko hili ili mnunuzi na muuzaji wawe wamekidhi vigezo vya kiasili, badala yake kila mtu anaingia sokoni vile atakavyo.
Hatari kubwa kwa vijana
Kwa kuwa leo hii hakuna anayesimamia soko la ngono, jamii imekubali kwamba hakuna tena umri sahihi wa kijana kuingia kwenye ngono. Kuanzia shule za msingi mpaka vyuoni, madrasa mpaka Sunday school, ndani ya familia mpaka mtaani, ngono imetamalaki. Wazee kwa vijana wanashindana kununua bidhaa. Lakini kuna hatari kubwa kwa vijana, inawaondolea focus ya matarajio yao ya baadaye, inavuruga kabisa mpangilio wa Maisha na kuwaingiza kwenye mtego wa kufuata malengo potofu (fake goals).
Leo hii lengo kuu la maisha sio procreation, yaani uumbaji, bali ni kujaribu kujistarehesha kwa kadri inavyowezekana. Ndio maana kumeibuka makundi kama watetezi wa kutoa mimba, watetezi wa mashoga n.k. Ndio sababu ya kustawi kwa biashara za vipodozi, kuongeza makalio, kuchubua mwili, nywele bandia n.k. (Kwa kawaida mwanamke akipindukia miaka 28 anatoka kwenye kundi la mabinti, umri unaanza kuwa dhahiri, hivyo matumizi ya vipodozi ili kujaribu kurejea huko anakopata soko kwa urahisi ni lazima. Ukimkuta binti mdogo anayefanya matumizi makubwa ya vipodozi utadhani kahaba, basi jua hiyo ni dalili ya kutojitambua.
Vijana wa kiume wanajaribu kujilinganisha na akina Fifty Cents ili wawavutie mabinti, badala ya kujikita kuandaa future zao. Unakuta matumizi ya make up yameongezeka kati ya vijana wa kiume. Zamani ilidhaniwa wanawake wanajipodoa ili kuwavutia wanaume, kumbe siku hizi hata wanaume nao wanajipodoa ili kuwavutia wanawake/wanaume!! Leo hii tuna beautiful men and women. Lol!!
Vijana wa kiume
Malezi ya kijana wa kiume yamelenga kumwandaa kuwa baba wa familia (wengine huona hili kuwa mfumo dume). Anaandaliwa kujitambua kuwa siku moja ataoa mke (wala sio kwamba ataolewa), mkewe atamzalia watoto, atakuwa na jukumu la kuwatunza mke na watoto, siku moja wazazi watahitaji matunzo yake, atakuwa na wajibu kwa jamii inayomzunguka n.k. Hivyo ni lazima awe na shughuli ya kumwingizia kipato. Hafundishwi kuwa mke wake atakuwa na shughuli ya kuingiza kipato kwenye familia, bali yeye mwanamume ndiye mwenye kutekeleza hilo.
Ili kufikia malengo hayo, kijana alitakiwa kujiepusha na mapenzi kabla ya wakati wake, kwani hii ingemtoa kwenye malengo yaliyokusudiwa. Akili ya kijana bado ni changa mno kuweza kuelewa tofauti kati ya kupenda na kutamani. Hajajua bado wajibu wake ama majukumu yanayoambatana na mapenzi, kwamba hayaishii kitandani tu. Pia hajui chungu ya mapenzi kwani ufahamu wake uko kwenye tamu tu.
Ngono ni kama madawa ya kulevya, ukionja mara moja utataka tena na tena. Leo hii vijana wameingia kwenye mtego wa kutamani kulala na wanawake wengi kadri wawezavyo kabla ya ndoa. wamebadili malengo kuwa kukidhi tamaa ya kimwili kuliko kujiandaa kuwa na familia. Wameingia kwenye ndoa bila kujua kuwa jambo hili litawatesa baadaye.
Kijana, unaposhiriki tendo la ndoa na mwanamke tayari unakuwa umeingia kwenye ndoa. Kifungo cha ndoa hakiwekwi kwa maneno kanisani, msikitini ama ofisini kwa kabidhi wasii mkuu wa serikali. Huko kote tunaweka ushuhuda tu, kwamba sasa hawa wawili wameamua kungana na hivyo mtu mwingine yeyote asiwaingilie. Ndoa halisi ni pale mnapojamiiana, mnakuwa kiumbe kimoja chenye uwezo wa kuzaa kiumbe kingine. Kulala na mwanamke nje ya ndoa ni kuingia kwenye ndoa isiyopangiliwa,ni kujiunganisha na mwanamke huyo na kumfanya sehemu ya maisha yako.
Unapolala na wanawake wengi unajiingiza kwenye vifungo vingi, huwezi kuelewa uhalisia wa mapenzi kwa vile wewe unafagia chochote kilicho mbele yako, ukijidanganya ni mapenzi. Unageuka mtumwa wa mapenzi (ndio kuingia kwenye ndoa) kwa kuanza kuwa baba wa familia kabla ya wakati husika. Vijana wengi walio kwenye mahusiano ya aina hii wanafanya yote ama baadhi ya haya kwa wapenzi wao:
1. kumpa pesa za matumizi
2. kumtibu akiugua
3. kumnunulia mavazi
4. kuwasaidia ndugu zake
5. kumpa muda wako
6. kumpa nguvu zako
7. kumpa mmoyo wako
8. kumlinda dhidi ya jambo lolote litakalomsibu
Kifupi ni kwamba umekuwa sehemu yake naye sehemu yako. Nafsi zenu zimeungana kiasi kwamba akiugua nawe unaugua, akipigwa yeye unaumia wewe. Hii ni ndoa kamili kwa sababu hayo yote ndio majukumu ya mume wa ndoa. Badala ya kujiandaa kuwa na ndoa njema, unaanza kutumikia ndoa nje ya ndoa, ndoa ya kikahaba. Badala ya kuwaza “long term” kama impasavyo mwanamume, unawaza mambo ya wakati huu, unaongozwa na unachokiona mbele yako, unakuwa mtumwa wa tamaa zako. Unawaza matako makubwa, waliochubua ngozi, wanaotoa nyuma, chuchu saa sita, mguu wa bia, nywele bandia, kwamba mwenye hayo ndio anayestahili muda wako na nguvy zako. Hizi ndizo gharama za soko huria la ngono, kila mtu anafanya akitakacho.
Vijana wa kike
Wanawake wengi hawawazi mambo ya siku zijazo (long term), wao wanatumikia emotions ama hisia zao. Huongozwa na kile kilichopo kwa wakati huo, kuliko kuwaza nini kitakuwa siku zijazo. Hii ndio sababu ya familia nyingi zenye kumjali binti huwa wakali sana kwenye malezi yake. Binti anapaswa kulelewa katika maadili ya kutunza familia, anapaswa kuandaliwa kuwa mke bora. Lengo kuu la ndoa ni uumbaji, ambapo mke na mume wanakuwa mwili mmoja wenye uwezo wa kutengeneza kiumbe hai. Ni kwa sababu hii imelazimu kuwapo mgawanyo wa majukumu ili mmojawapo wa wanandoa awe msimamizi wa viumbe vinavyozaliwa katika familia.
Binti akijiingiza kwenye mapenzi kabla ya wakati ni sawa na kujiweka sokoni tayari kwa wateja. Kwa kuwa hajajua misingi ya mapenzi na nini kinatarajiwa toka kwake, mara nyingi hawezi kujua mtu sahihi kwake, kwani walio sahihi hawana mbwembwe nyingi kama mbwa mwitu. Atabebwa na kile kinacho trend wakati huo, kama ni kijana mwenye buga, ama tattoo, ama aliye bleach nywele, ama aliyeacha boxer nje, ama aliyetoga masikio n.k. Kwa binti huyu, mwanamume bora atategemea kitu gani kinavuma kwa wakati uliopo. Atatumia uchi wake kama silaha ya kujaribu kumtawala mwanamume lakini mwishowe mahusiano huvunjika na hivyo kujikuta akihama toka mwanamume mmoja kwenda mwingine na mwingine.
Mwanamke akitembea na wanaume wengi hutengeneza emotional blur, hali ya kujiunganisha na kudumu na mwanamume mmoja hupotea ama kupungua sana. Ni kwa sababu ya spiritual bond inayokuwepo kati ya mwanamke na mwanamume wanapojamiiana. Muunganiko huu una nguvu kubwa sana kwa mwanamke tofauti na mwanamume. Ukitaka kuthibitisha hili angalia, mwanamume anaweza kutumia mwaka mzima na mali nyingi kumtongoza mwanamke, akiisha kulala naye akawa hana mpango naye tena. Lakini mwanamke akilala na mwanamume huuelekeza moyo wake wote huko, huwa na kusudio la kuwa na mahusiano ya muda mrefu.
Kwenye mahusiano wanawake wanawaza long term mpaka pale wanapotembea na wanaume wengi, lakini wanaume wanawaza short term mpaka pale wanapokomaa kifikra na kimtazamo kuhusu maisha. Mwanamke aliye mwanamwali atawaza ni jinsi gani apate mume wa kumtunza wazae watoto wawalee vema wazeeke pamoja kama mke na mume. Pale atakapojiingiza kwenye ngono za mapema tu, malengo hugeuka kuwa ya muda mfupi, apate mwanamume wa kumnunulia chips, vipodozi, kumpeleka club, kumnunulia mavazi n.k. Hata lijapo wazo la ndoa huwa ni vague (halieleweki) kwa sababu atasema anatafuta mwanamume wa kumuoa wakati huo huo ana maboyfriend watatu ambao ameona hawana mpango wa kumwoa. Hawa anawatumia kama wanaume wa muda wa mpito (transition period) mpaka pala atakapompata wa kutaka kumuoa.
Mwanamume anayechipukia muda wote atawaza namna ya kuwavutia wanawake apate mabinti walio warembo, apate kusifiwa na wenzake kwa kujichukulia pisi kali!![/I][/B]. Atatafuta kutumikia matakwa ya jamii iliyokwisha kuharibika na kuona mambo ya kijinga kuwa ndio fahari, hivyo yeye pia kuwa kati ya wajinga. Asipopata maongozi sahihi akajiingiza kwenye mapenzi ya mapema, ataishi kwa kutumikia hayo na akili yake itashika uelekeo huo tu. Pale atakapokuja kukomaa kiakili na kuona kuwa amekosea njia kutokana na ukweli wa maisha, ndipo ataanza kutazama siku za mbeleni maisha yatakavyokuwa.
Baada ya kuonja na kupitia mitindo mbalimbali ya ngono ni vigumu sana kwa mwanamke kuamua yupi ni mwanamume sahihi kwake kwa vile kila mmoja ana kionjo tofauti na mwingine. Hali hii ataingia nayo hata kwenye ndoa na inasababishwa na emotional blur. Emotional blur kwa mwanamke ina nguvu sana kwa sababu wanawake ni emotional beings, wanaendeshwa na hisia zao. Ukiona mwanamume anaendeshwa na hisia ujue huyo amepoteza mwelekeo. Kwa upande wake mwanamume akikomaa ni rahisi kuamua kujikita kujenga familia kwa kujitafutia mwanamke anayedhani atamfaa kwa wakati huo.
Baada ya muda, binti huyu hubadilika kutokana na mtazamo wa jamii, hutafuta kutoka na watu wenye hadhi fulani katika jamii. Hapo ndipo unakuta rundo la wanawake wakigombea penzi la mwanamume mmoja, hii inaitwa hypergamy. Zaidi ya 80% ya wanawake wanagombea chini ya 20% ya wanaume kwa sababu ya social status zao. Ndio maana utaweza kuona mwanamume mmoja amezungukwa na mabinti watano akistarehe nao utadhani mifugo yake. Wanawake wa aina hii wamepoteza mwelekeo, watajenga mahusiano na wanaume ambao hawana mwelekeo, watazaa watoto wasio na mwelekeo kutokana na aina ya malezi.
Kwa sababu wanawake hujiingiza wenyewe sokoni kwa kuwa jamii hai – regulate soko la ngono, hujikuta wakitumika kama vyombo vya kuwastarehesha wanaume wenye kiu, mwishowe huachwa wakiwa hawajui la kufanya, wengine wakiwaa single mothers, wengine hawana tena ule mvuto kwa hao hao wanaume waliowatumia, badala yake huwanyooshea vidole wanaume kwa makosa yao wenyewe.
Pale mwanamke huyu anapodhani amejitambua na kutafuta mwanamume wa kumwoa muda unakuwa umekwenda. Ni mara chache sana kwa mwanamume kumrudia mwanamke wa aina hii kwani uzoefu alionao ni hatari kwa mustakabari wa ndoa, na hapo ndio utaona wanaume wa umri mkubwa wakioa mabinti wadogo. Kundi hili la wanawake ndilo linaloongoza kwa kupiga makelele pale mwanamume wa miaka 45 anapooa binti wa miaka 25 kwamba ameacha wanawake wa umri wake akaoa mtoto wake. Ukweli ni kwamba anajiuliza kama wanaume wa rika lake wanaoa mabinti wachanga, yeye ataolewa na nani? Ni wivu tu, hakuna Zaidi. Kuna msemo mmoja wa kiingereza, a man is as old as he feels, a womana is as old as she looks!! Baada ya kuuchezea ujana, anakumbuka shuka wakati kumekucha.
Umri wa binti kutamba ni kati ya miaka 18 mpaka miaka 28, huo ndio wakati sahihi wa kujitafutia mume mwema na kuwa na dnoa imara. Sio wakati wa kutumika kuwastarehesha wanaume kwani miaka 10 ni muda mfupi mno! Ni kipindi ambacho binti mwenye maadili mema anajipambanua na thamani yake halisi kuonekana. Ni wakati huu mwanamume mwenye nia ya dhati kupata mke anapoamua kuwa binti huyu amekidhi vigezo vya kuwa mke kwa jinsi ambavyo ameishinda social pressure na kuwa na msomamo bora wa kimaadili. Ni wakati ambao maisha ya baadaye ya binti huyu yanategemea. Tatizo kubwa ni kuwa jamii haina tena ule uwezo wa kumlinda kwa sababu ya matakwa yake ya usawa, jamii imeondoa ulinzi na kumpa kile akitakacho na ndicho kinachomwangamiza. Zamani watu walifanya mapenzi vichakani kwani kulala gesti mume na mke ilihitaji cheti cha ndoa. Ni nyakati ambazo mwanamume kuonekana umesimama na binti katika hali isiyoeleweka lilikuwa kosa la kukuingiza matatani dhidi ya jamii. Lakini tangu mwanamke alalamikie ulinzi aliopewa na jamii kuwa ni unyanyasaji, serikali za dunia zimengilia kati ili kumkomboa mwanamke huyu na sasa anatumbukia kwenye shimo alilochimba mwenyewe.
Wazazi kama wasimamizi wa soko la ngono
Kama nilivyogusia, wazee ndio waliokuwa na jukumu la kusimamia (to regulate) sooko la ngono. Mamlaka hayo yameporwa na serikali na sasa uwanja umewekwa wazi, ndio maana tuna age of consent (umri unaokubalika kisheria kujiingiza kwenye vitendo vya kingono). Kwamba kijana anapofika umri huo ni halali kisheria kujiingiza kwenye ngono bila kujali ameolewa ama la. Hapo mzazi hana uwezo wa kuchukua hatua yeyote labda kama sheria ya elimu iliyotungwa baada ya ubazazi kuongezeka imevunjwa. Vijana ambao bongo zao hazijakomaa kuweza kutambua yajayo wanapewa uhuru wa kuamua kuhusu maisha yao ya baadaye.
Sasa badala ya wao wenyewe kuamua, wanaanza kujifunza huko ulaya na marekani wanafanyaje? Hawahitaji tena kuwaangalia wazazi wao walifanyaje mpaka kufikia hapo walipo, wanahamia kuiga tamaduni za nje. Ndipo hapo tunapopata kizazi ambacho ni nusu wanaume nusu wanawake! Wanaume wanaotunzwa na wake zao, wanaotoga masikio na pua, wanaoacha chupi nje, wanaoweka make up, wanaojichubua ngozi, wanaokalikiti nywele zao, mashoga n.k. ndipo hapo tunaona wanawake wakivuta sigara, wakivaa kiume, wakichora tattoo, wakikesha club wakitumikia ulevi, wasagaji n.k.
Wazazi kama hatutaamka na kurejea miiko etu, kama tutaendelea kuruhusu hali hii iendelee, tujue kuwa tutakuwa na kesi ya kujibu mbele za Mwenyezi Mungu. Tumepewa watoto kwa maana kwamba tuwalee katika maadili mema, lakini badala yake tumeruhusu dunia iwale itakavyo. Imetupasa tutubu turejee ulikotoka.
Bahati mbaya san ahata kwenye Imani zetu dunia ndio inavirekebisha vitabu vitakatifu na sio vitabu hivyo kuirekebisha dunia. Misikitini watu wanasafisha vikombe kwa nje lakini kumbe ndani ni uozo mtupu, makanisani wao sasa hata kusafisha kwa nje tu imeshindikana. Ukiona kusanyiko linatoka kanisani utashindwa kuelewa kama ni makahaba waliosikia injili kwa mara ya kwanza au ni waumini wazoefu! Sitaki kuliongelea hili kwenye thread hii kwani litawatoa wadau kwenye kusudi halisi.
Commentaires