MASWALI YA KUJIULIZA KABLA YA KUOWA
1 Maswali Kuhusu Mambo ya Msingi.
1.Je! Mmejuana kwa muda gani?
2.Mmekuwa pamoja kwa kiasi gani?
3.Mlikutanaje?
4.Mmefanya mambo gani mkiwa pamoja?
5.Je! Familia zenu na rafiki 6.wanafikirije kuhusu uhusiano wenu? 7.Wanaonyesha wasiwasi wao kuhusu nini?
8.Mngetaka kuoana lini?
9.Nini masharti ya kisheria ambayo 10.lazima yatimizwe?
11.Nini wasiwasi wako unapofikiri 12.kuingia katika ndoa na huyu? Je! Kwa 13.sasa anakutendaje?
2) Maswali Kuhusu Maisha ya Kiroho
1.Je! Wote wawili ni waaminio? 2Kor 6:14-16 nuru haipaswi kuwa na giza.
2.Je! Mnakuwa katika imani? Kuna 3.ushahidi gani kuwa ni kweli?
4.Je! Mnatabia gani?
5.Je! Mnakubaliana kuhusu mamlaka ya maandiko na itikadi kwa ajili ya maisha yenu? Namna ya kutendeana, na kuwalea watoto (Ef. 5:21-6:4; Kol. 3:17-21; 1Pet. 3:1-7).
6.Je! Mnajua kinachofundishwa na Biblia kuhusu ndoa?
7.Je! Mmeomba kuhusu uamuzi huu?
8.Mtakuwa mnaabudu wapi?
9.Mnatazamia kusaidiaje katika kanisa hilo?
3) Kwanini mtu asiingie kwenye ndoa na mtu anayekasirika na kulaumu sana?
Maswali yahusuyo hali nzuri ya moyo
1.Je! Mhusika anapenda kulaumu?
2.Je! Mhusika ni mwenye furaha?
4) Maswali Kuhusu Mahusiano
1.Je! Mhusika anahusianaje na watu wengine?
2.Anatendeaje wazazi, ndugu, watoto, walio karibu naye n.k.
3.Je! Unajua kuwasiliana vizuri wakati wa maongezi
4.Mawasiliana si kuzungumza tu, hata kusikiliza, kutafauta kuelewa mitazamo tofauti.
5.Mwanamke usikubali kuolewa na mtu aliyenyamaza kimya kama mti!!!
5) Maswali Kuhusu Hali ya Afya Kihisia
1.Unapenda nini juu ya afya yako mwenyewe? Je! Ungependa kubadilika na kuwa mtu mwingine? Nani? Eleza jibu lako.
2.Umewahi kukasirika? Unapokasirika unafanya nini?
3.Mnajisikiaje juu ya wazo la kushirikishana mawazo yenu na hisia zenu?
4.Nini sababu tano za kutaka mwoane? (isiwe kwa kutaka kutatua tazio Fulani binafsi, au kumpendeza mtu fulani).
Unafanyaje kuhusu mabadiliko?
5.Unahusianaje na ndugu na dada zako?
Eleza mahusiano yako na wazazi wako. 6.Je! Kuna mmoja au zaidi kati ya wazazi wakoanayejaribu kukutawala? Eleza jibu lako.
7.Je! Unayetaka kuoana naye huonyesha huzuni baada ya kufanya kitu kisichofaa? Je! Ana uwezo wa kushinda hatia na kusonga mbele?
8.Je! Umefungwa kwa namna yeyote, au una tabia zozote zilizokufunga?
9.Hebu eleza jinsi unavyofanya maamuzi. Eleza juu ya uamuzi uliofanya juma hili. Eleza juu ya uamuzi muhimu u liowahi kufanya. Uliamuaje?
10.Je! Unaweza kushughulika na hali halisi? Ana busara au hana? Je! 11.Anafikiri kuhusu matokeo? Je! 12.Anafikiri juu ya wengine?
6) Maswali Kuhusu Matarajio
Je! Unaamini ndoa ni kujitolea hadi 1.kufa?
2. Nin sababu za watu kuachana?
3. Mume mzuri yukoje? Hebu eleza kidogo juu yake.
4. Mke mzuri yukoje? Hebu eleza kidogo juu yake.
5. Je! Mtatumia muda gani kuwa pamoja?
Mnapokuwa na nafasi huru, mtafanya nini mkiwa pamoja?
6. Je! kutakuwepo na wakati ambapo kila mmoja wenu atakuwa huru kuwa na muda wake binafsi?
7. Mnafikiri kiwango chenu cha mapato kimaisha kitakuwaje?
8. Je! Unamtazamia mwenzio afanye kazi za namna gani?
9. Je! Wote wawili mnatazamia kuwa na kipato?
10. Unatazamia mwenzio kuwa hadhi gani katika jamii?
11. Mtakuwa mnatumiaje nyakati zenu za likizo? Ikiwa wote mmeajiriwa.
12. Unatazamia kushirikiana vipi na familia ya mwenzako?
13. Mwenzako atakuonyesha vipi upendo na heshima? Unatazamia akuonyeshe vipi hayo?
14. Je! Kwa maoni yao, Waefeso 5:22-33 itafanyaje kazi katika ndoa yako?
15. Unatazamia mwenzako aonyeshe vipi 16. huzuni kwa kukuumiza?
18. Mume wako au mke wako atajuaje kuwa kuna kitu kinachokusumbua?
19. Mnatazamia kushirikishana kiasi gani mawazo na hisia zenu?
20. Mtafanyaje maamuzi kuhusu maisha yenu kwa pamoja?
21. Mtaishi wapi?
7) Maswali Kuhusu Afya na Mwili?
1. Je! Afya yako ni nzuri?
2. Je! Una matatizo ya muda mrefu kiafya?
3. Je! Unamatatizo yanayotokana na ngono? Umepimwa?
4. Je! Unaelewa mwili wako vizuri, na mambo yanayohusiana na ngono? (Fafanua ikibidi).
5. Je! Itakuwaje iwapo mmoja wenu atapata kilema au kuwa mgonjwa sana?
8) Maswali kuhusu Watoto
1. Je! Mngependa kuwa na watoto wangapi?
2. Mna mipango gani kuhusu uzazi wa mpango?
3. Je! Mnathamini watoto wa kiume na wakike sawasawa?
4. Mngependa kupata watoto lini baada ya kuoana?
5. Je? Mna watoto tayari? (kama ndivyo, wataishi nanyi? Wanajisikiaje kuhusu ndoa yenu? Mnawaandaaje kuhusu ndoa hii?).
6. Baada ya kuoana nani atakayekuwa anaadhibu watoto?
7. Je! Unatazamia mwenzako ashirikiane vipi na watoto?
8. Taja njia inayofaa uadhibu watoto? 9. Je! Wazazi wako walikuadhibuje wewe?
Eleza aina ya uhusiano unaotaka mwenzako awe na watoto wenu.
Mnataka watoto wenu wapate elimu ya aina gani?
Mngependa watoto wenu washirikiane vipi na familia zenu?
Itakuwaje kama hamtaweza kuwa na watoto?
9) Maswali Kuhusu Mambo ya Ngono
1. Je! Mwenzako anakujaribu? Je!
2. Anajitahidi kutosheleza shauku yako ya ngono?
3. Unatarajia nini katika mambo ya ngono?
4. Je! Umepata mafundisho juu ya maswala ya ngono?
5. Nini mpango wenu wa kubakia safi kwa habari ya ngono mpaka wakati wa ndoa? 6. Je! Mmefuata mpango huo?
7. Je! Umewahi kukutana kimwili na mtu yeyote?
8. Je! Una “picha au sinema chafu” za aina yeyote? (au, unatumia?)
9. Je! Umewahi kunyanyaswa kingono?
10. Je! Kusudi pekee la ngono ni kupata watoto? Je! Ni sawa kufurahia ngono katika ndoa?
10) Maswali juu ya Vinavyothaminiwa na wote, na tofauti za wote.
1. Umri wenu?
2. Mlikulia wapi?
3. Mnatoka kabila gani/jamii gani?
4. Je! Wazazi wote wawili wapo?
5. Je! Ulilelewa na wazazi wote?
6. Familia yenu ni dini gani?
7. Vipi hali ya kijamii na kifedha ya familia yenu?
8. Umesoma hadi kiwango gani? Nini
9. mipango yako ya baadaye kuhusu elimu?
10. Je! Nyumba iwe safi kiasi gani? Na mtu binafsi je! Awe safi kiasi gani?
11. Unapenda vyakula gani zaidi?
12. Unapenda kuthubutu kujaribu vitu, au unapenda kuwa mwangalifu?
13. Je! Unapanga mambo mapema, au unapenda kufanya mambo ghafla?
14. Je! Unapenda kuwa na watu wengi, au ungependa kuwa nyumbani?
15. Je! Wewe ni mkimya au wewe ni mzungumzaji sana?
16. Je! Wewe ni rahisi kushirikisha hisia zako, au ni mtu anayekaa na mambo yake binafsi?
17. Hebu eleza mafanikio – ni nini? Ni muhimu kiasi gani kwako?
18. Maoni ya watu wengine ni muhimu kiasi gani kwako?
19. Ni nini cha muhimu zaidi kuhusu urafiki?
20. Ni mambo gani matatu yanayokuvutia zaidi?
21. Kama ungeweza kupata kazi, ungechagua ipi? Je! Unaelekea huko?
11) Maswali Kuhusu Fedha
1. Je! Wewe ni mchapa kazi hodari?
2. Una madeni yeyote?
3. Je! Una kazi?
4. Je! Una kiasi katika kununua vitu? 5. Au unanunua vitu usivyohitaji?
6. Umeweka akiba gani ya kuleta kwenye ndoa?
7. Je! Una bajeti?
8. Unapataje fedha? Unapata kiasi gani?
9. Mtafanyaje maamuzi kuhusu fedha?
10. Mnajisikiaje kuhusu mikopo na madeni?
11. Nini malengo yenu kifedha?
12. Je! Vitu ni muhimikiasi gani kwenu?
13. Mtu mkarinu yukoje? Je! Wewe ni mkarimu?
14. Unatoa fungu la kumi?
15. Je! Umewahi kuweka ahadi ya imani kwa ajili ya utume?
16. Je! Mke na mume washirikishane fedha yao yote na mali yao?
17. Je! Ni sawa kwa majina ya yao wate kuwa kwenye hati ya nyumba au shamba?
18. Nani atakayesimamia fedha katika familia?
19. Je! Wote wawili mtajua kuhusu fedha za familia?
20. Je! Unatabia za kupenda michezo ya kubahatisha (kamari)?
21. Je! Unakawaida ya kuingiza fedha zako kwenye mambo ya “pata potea”?
Commentaires