Kwa nini kuna shimo lisilo la kawaida katika tabaka la ozoni?
Tangu 2011 hakujawahi kuwa na tukio kama hilo.
Tangu robo ya mwaka uliopita, shimo lisilo la kawaida lenye urefu wa kilomita 18 lilijitokeza angani katika tabaka la ozoni ya eneo la kaskazini zaidi la dunia la Arctic, kama ilivyoripotiwa na shirika la anga za juu la ulaya CAMS wiki iliyopita.
Tukio kama hili ni la kawaida katika eneo la kusini zaidi la dunia la Antarctic wakati wa msimu wa joto, lakini katika eneo la baridi la kaskazini si la kawaida.
Uchunguzi wa tabaka la ozoni ni muhimu kwa sababu inatulinda dhidi ya miale mikali ya ya jua duniani.
Katika eneo hilo ardhi na milima iliopo inaathiri mabadiliko ya hali ya hewa ili vipimo vya joto visishuke kama ilivyo katika eneo la Antarctic.
Hata hivyo maeneo mengi ya eneo la Arctic yameandikisha rekodi ya vipimo vya baridi ndogo zaidi mwaka huu huku tabaka la ozoni ya anga ya eneo la Arctic ikiathiriwa kwa urefu wa kilomita 18.
Tangu msimu wa joto wa 2011, hakujawahi kutokea uharibifu wa tabaka la ozoni wa kiwango kama hicho katika eneo la Arctic.
Tobo katika ‘paa la dunia’ laendelea kujifunga
Na wasayansi wa shirika la CAMS wanasema kwamba mwaka huu 2020 uharibifu huo wa ozoni utakuwa zaidi.
Je mashimo hayo hujiunda vipi?
Shimo la Ozoni katika eneo la Antarctica linatokana na kemikali za wanadamu kama vile chlorine na bromine ambazo humwaywa katika mazingira.
Kemikali hizo hujikusanya katika eneo la baridi.
Porlar Votex ni eneo kubwa lisilo na hewa ya kutosha ambalo limezunguka maeneo ya baridi duniani.
Hali hii hupungua katika msimu wa joto na kuimarika katika msimu wa baridi, kulingana na afisi ya kitaifa kuhusu usimamizi wa masuala ya baharini na angani NOAA.
vipimo vya joto vya eneo la Vortex vinaweza kushuka hadi -78 ° C na kutengeza mawingu ambayo huwa na jukumu muhimu katika kukabiliana na kemikali zinazotengenezwa na wanadamu ambazo uharibu anga ya ozoni wakati jua linaporudi,
kulingana na utafiti huo wa CAMS .Ijapokuwa uharibifu huo wa anga umefanyika kwa kikpindi cha miaka 35 iliopita, shimo lililojitokeza 2019 ni dogo zaidi kuwahi kuonekana
Viwango vya baridi vya muda mrefu
Kuhusiana na shimo hilo la Arctic mwaka huu , wanasayansi wanaelezea kwamba viwango vya chini vya baridi vya miezi kadhaa vimesababisha kuundwa kwa mawingu katika eneo la kaskazini la nusu ya dunia hatua inayosababisha uharibifu wa muda mrefu wa anga ya ozoni.
Kiwangio kama hiki cha uharibifu wa ozoni kinatokana na baridi kali ya muda mrefu , takriban siku 10 zaidi ya ilivyo kawaida, kulingana na Oscar Dindore Miles wa maabara ya fizikia ya angani kutoka Chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza.
Haki miliki ya pichaGETTY
Image caption
Porlar Votex ni eneo kubwa lisilo na hewa ya kutosha ambalo limezunguka maeneo ya baridi duniani.
Hatahivyo CAMS imehakikisha kuwa eneo la baridi la Arctic limesalia kuwa "la kipekee, dhabiti na linaloweza kudumu kwa muda mrefu".
"Utabiri wetu ni kwamba viwango vya joto vimeanza kushuka katika eneo la porlar ya vortex , anasema Vincent-Henri Peuch, mkurugenzi wa CAMS
Mshindi wa tuzo ya Nobel kutoka Mexico Mario Molina: "anga ya ozoni ni mfano muhimu wa tatizo duniani ambalo linaweza kusuluhishwa kwa ufanisi mkubwa.
Hii inamaanisha kwamba uharibifu wa anga ya ozoni unaweza kupunguza kasi na kusitishwa kabisa,
Wakati upepo unaotoka eneo la baridi unapochanganyika na uupepo wa ozoni kutoka latitude ya kiwango cha chini , aliongezea mwanasayansi huyo.
Hapo pia ndipo anapoungwa mkono na Dimsdore Miles anayesema kwamba wakati Vortez ya eneo la baridi inapopasuka, tukio linalofanyika kila mwaka mwezi huu, viwango vya ozoni hujipona katika kipindi chote cha mwaka kilichosalia.
''Tutaendelea kuchunguza shimo hilo la ozoni katika kipindic cha wiki zijazo . ni muhimu sana kuimarisha juhudi za kimataifa ili kuchunguza mashimo ya ozini kila mwaka pamoja na anga ya ozoni'' ,alimalizia Vincent peuch.
Commentaires