Coronavirus: Kwa nini shirika la afya duniani linasema hatua ya kujishika uso ni hatari kwa maisha yako?
Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii WhatsApp Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Twitter Mshirikishe mwenzako
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Sote hushika macho, mashavu. kidevu na mdomo mara kadhaa kila siku
Kati ya tabia zote zinazotutofautisha na wanyama duniani kitu kimoja kinatutia wasiwasi wakati wa milipuko ya magonjwa.
Sisi ndio spishi inayoweza kushika nyuso zetu bila kugundua. Na hilo linasaidia kusambaza magonjwa kama vile coronavirus Covid-19.
Kwanini tuna tabia hiyo na ni hatua gani tunayoweza kuchukua ili kuisitsha?
Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na coronavirus yaongezeka Italia
Je, ni taarifa gani feki zinazoenezwa Afrika kuhusu coronavirus?
Marufuku kupeana mikono, busu katika nchi hizi
'Kushika uso'
Sote tunashika nyuso zetu mara kadhaa. Utafiti uliofanywa 2015 ambao uliangazia wanafunzi wa matibabu nchini Australia ulibaini kwamba hawawezi kujizuia.
Pengine wanafunzi wanaojifunza masuala ya matibabu wanapaswa kuwa na hamasa kuhusu hatari zaidi ya wengine, lakini waligusa nyuso zao sio chini ya mara 23 kwa saa, ikiwemo kushika mdomo, pua na macho.
Bodi ya afya ya umma na wataalam , ikiwemo Shirika la Afya duniani WHO zinasema kwamba tabia hiyo ni hatari.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Macho yetu, pua na mdomo ndio mlango wa viini kuimbia mwilini mwetu
Ushauri wa maradhi ya Covid-19 unasisitiza umuhimu wa kuzuia mikono yetu mbali na wasiwasi kwamba ni michafu.
Kwa nini tunalazimika kufanya hivyo?
Wanadamu na wanyama hawawezi kujizuia kutokana na jinsi tulivyobadilika na kuwa.
Huku wanyama wengine wakishika nyuso zao ili kuwatishia wanyama wengine, sisi na wanyama wengine hushika nyuso kwa sababu za kila aina.
Mara nyingine ni jambo la kutaka kujiliwaza, kulingana na Dacher Keltner - profesa wa Psychology katika chuo kikuu cha UC Berkeley nchini Marekani, mara nyengine tunatumia tabia ya kushika uso ili kuvutia jinsia nyengine.
Wataalam wengine katika sayansi ya tabia wanasema kwamba kujishika ni njia moja ya kuzuia hisia. Martin Grunwald , mwanasaikolojia wa Ujerumani katika chuo kikuu cha Leipzig, anasema ni tabia ya spishi zetu.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Wanadamu na sokwe ndio spishi za pekee wanojulikana kujigusa kwa sababu za kuwagopesha adui zao
"Kujishika ni tabia za kawaida ambazo hazilengi kuwasiliana na hufanyika bila mtu kujua, Grunwald aliambia BBC.
'' Zinachukua jukumu muhimu katika utambuzi na mchakato wa hisia. Hujitokeza katika kila mtu'' , aliongezea profesa, ambaye ni mwanzilishi wa kitabu cha 2017 cha Homo Hapticus.
Kwa nini hatuwezi kuishi bila kujigusa uso. Tatizo la kujishika ni kwamba macho, pua na mdomo ndio milango ya vitu vyote vibaya.
Codi- 19 kwa mfano , husambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine kupitia matone madogo yanayotoka puani ama mdomoni kutoka kwa mtu aliyeambukizwa.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Kugusa sakafu ambazo zimeguswa na virusi hivyo kunaweza pia kusababisha maambukizi
Lakini maambukizi pia hutokea baada ya kushika sakafu ambazo zina viini vya virusi hivyo.
Huku wataalam wakiendelea kujifunza kuhusu virusi hivi vipya , coronavirus hujulikana kuwa virusi visivyoisha nguvu na vingine vimejulikana kuishi katika sakafu kwa hata zaidi siku tisa.
Uwezo wa kuishi
Uwezo wake wa kuishi huvifanya kuwa hatari wakati mtu anapojishika uso.
Mwaka 2012, watafiti wa Marekani na Brazil walibaini kwamba watu kadhaa walishika sakafu za maeneo tofauti zaidi ya mara tatu kila saa.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Barakoi zinaweza kulinda nyuso zetu
Pia walishika midomo yao na pua takriban mara 3.6 kila saa.
Hii ni chini ya kiwango cha mara 23 kwa saa kwa wanafunzi wa matibabu wa Australia , pengine kwa sababu walikuwa wakiendelea na masomo badala ya kuwa nje ambapo wangekuwa wakifanya mambo mengi tofauti.
Kwa wataalam wengine wa afya, suala la kujishika ndio sababu kuu ya watu kutumia barakoa kama njia ya kujilinda dhidi ya virusi hivyo.
Kuvaa barakoa kunaweza kuzuia kiwango cha watu kujishika uso, ambacho ni chanzo kikuu cha maambukizi iwapo mtu hajaosha mkono, Stephen Griffin wa chuo kikuu cha Leeds, alielezea.
Je ni hatua gani tunazofaa kuchukua?
Lakini je ni hatua gani tunazoweza kuchukua ili kuweza kupunguza wepesi wa tunavyogusa nyuso zetu?
Mwanasayansi wa masuala ya tabia Michael Hallsworth, profesa wa chuo kikuu cha Colombia ambaye alifanya kazi kama mshauri wa sera katika serikali ya Uingereza chini ya aliyekuwa waziri mkuu David Cameron , anaelezea kwamba ni vigumu kufanya ushauri kuwa kitendo.
''Kuwaambia watu kufanya kitu ambacho hutokea bila wao kujua ni tataizo kuu'', aliiambia BBC.
''Ni rahisi kwa watu kuosha mikono yao mara kwa mara badala ya kugusa nyuso zao mara chache. Hautafanikiwa iwapo utamwambia mtu usifanye kitu asichokijua''.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Unawezaje kusitisha kufanya kitu usichojua unakifanya?
Hallsworth, hatahivyo anaamini kwamba kuna mbinu ambazo zinaweza kutumika.
Mojawapo ni kujali ni mara ngapi sisi hushika nyuso zetu. Iwapo ni hitaji lisiloepukika kama vile kujikuna, kwa mfano tunaweza kufanya kitu kingine.
Tumia nyuma ya mgongo wa mkono kujikuna. Unapunguza hatari hata iwapo sio suluhu ya kudumu.
Kubaini kinachotufanya kushika nyuso zetu.
Mtaalam wa tabia pia anapendekeza kubaini ni kwa nini tunajishika.
''Iwapo tutabaini sababu ambazo zinatufanya kujishika, ni swala tunaloweza kulifanyia kazi'' , Hallsworth anaelezea.
Watu wanaoshika macho yao wanaweza kuvaa miwani. ama kukalia mikono yao iwapo wanahisi huenda wakajishika.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Njia pekee ya kuzuia maambukiz ni kuosha mkono mara kwa mara
Pia tunaweza kutumia mbinu ya kuifanya mikono yetu kuwa na shughuli nyingi - wakati ambapo vidole vyetu havina kazi ya kufanya. lakini ni muhimu kuosha mikono mara kwa mara.
''Kujikumbusha kutoshika ama kugusa uso kunaweza kukusaidia. Iwapo mtu anajua kwamba ana tabia za kujishika wanaweza kuwashauri marafiki ama ndugu kuwaonya'', alisema Michael Hallsworth.
Je kuvalia glavu kama kikumbushi? Iwapo tabia mbaya hazitabadilishwa ama kuoshwa mara kwa mara kama mikono pia zinaweza kusababisha maambukizi.
Kuosha mikono kunasaidia
''Mwisho wa siku, hakuna kitu muhimu zaidi ya kuosha mikono. Hatuna haja ya kusubiri chanjo na matibabu'' , alisema mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani Tedrod Adhanom Ghebreyesu katika mkutano na vyombo vya habari tarehe 28 mwezi Februari.
''Kuna vitu ambavo kila mtu anaweza kujilinda na wengine leo'', Dkt Tedrod aliongezea.
Commentaires