Kwa nini kuna shimo lisilo la kawaida katika tabaka la ozoni?
Tangu 2011 hakujawahi kuwa na tukio kama hilo. Tangu robo ya mwaka uliopita, shimo lisilo la kawaida lenye urefu wa kilomita 18 lilijitokeza angani katika tabaka la ozoni ya eneo la kaskazini zaidi la dunia la Arctic, kama ilivyoripotiwa na shirika la anga za juu la ulaya CAMS wiki iliyopita. Tukio kama hili ni la kawaida katika eneo la kusini zaidi la dunia la Antarctic wakati wa msimu wa joto, lakini katika eneo la baridi la kaskazini si la kawaida. Uchunguzi wa tabaka la ozoni ni muhimu kwa sababu inatulinda dhidi ya miale mikali ya ya jua duniani. Katika eneo hilo ardhi na milima iliopo inaathiri mabadiliko ya hali ya hewa ili vipimo vya joto visishuke kama ilivyo katika eneo la Antarctic. Hata hivyo maeneo mengi ya eneo la Arctic yameandikisha rekodi ya vipimo vya baridi ndogo zaidi mwaka huu huku tabaka la ozoni ya anga ya eneo la Arctic ikiathiriwa kwa urefu wa kilomita 18. Tangu msimu wa joto wa 2011, hakujawahi kutokea uharibifu wa tabaka la ozoni wa kiwango kama hich...