Coronavirus: Nchi za Muungano wa Ulaya zarekodi idadi ya juu ya vifo vinavyotokana na virusi vya corona Dakika 29 zilizopita
Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii WhatsApp Sambaza habari hii Messenger Mshirikishe mwenzako
Haki miliki ya pichaEPA
Nchi tatu zilizo na kiwango kikubwa cha watu walioambukizwa virusi vya Corona barani Ulaya zimerekodi idadi kubwa ya vifo kwa siku.
Italia ilikuwa na idadi ya vifo 368 na kufanya idadi yao kufikia 1,809, Uhispania ikarekodi vifo 97 zaidi na kufikia 288, huku Ufaransa ikiripoti vifo 29, na kufikisha idadi ya waliokufa hadi 120.
Uingereza pia imeshuhudia ongezeko la idadi ya vifo vipya 14 na kufikisha jumla ya 35.
'Wajerumani katika hatari ya kuambukizwa Coronavirus'
Trump azuia safari za kutoka Ulaya kuingia Marekani
Serikali za nchi nyingi zanchi wanachama wa Muungano wa Ulaya zimechukua hatua kwa kuweka masharti ya uhuru wa kusafiri kwa wanaoingia kuimarisha mipaka yao.
Mfano Ujerumani imedhibiti mipaka yake na Ufaransa, Uswizi, Austria, Denmark na Luxembourg kuanzia Jumatatu asubuhi huku Ureno ikifunga mpaka wake na Uhispania.
Serikali ya Czech imeanzisha hatua kali: Watu wataruhusiwa tu kwenda na kutoka kazini na kununua chakula na dawa na kutembelea familia kwa dharura lakini uhuru wa kusafiri utadhibitiwa kwa kiasi kikubwa kuanzia Jumapili usiku hadi Machi 24.
Austria inaanza kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya watano kuanzia Jumatatu na Jamuhuri ya Ireland imeagiza baa zote kufungwa kuanzia Machi 29.
Shule zitafungwa katika nchi nyingi za Ulaya.
Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa sasa limetangaza Ulaya kama kitovu cha janga hili la Corona ambao chimbuko lake ni China.
Virusi hivi vimesambaa kiasi gani?
Kwa kuangazia ukubwa kwa janga hili, Uswizi ilitangaza kwamba maambukizi yaliongezeka kutoka 800 hadi 2,200 kwa saa 24 peke yake. Nchi hii imerekodi visa 14 vya vifo.
Italia imeathirika kwa kiasi kikubwa na janga hili ikiwa na maambukizi 24,747 huku 1,218 wakiaga dunia katika eneo moja la Lombardy, ambalo ni kama kaya kwa eneo ambalo ni kitovu cha biashara la Milan.
Serikali imesitisha shughuli zote nchini humo kuanzia Jumatatu iliopita, watu hawaruhusiwi kutembea na pia imeagiza maduka yote yafungwe isipokuwa ya chakula tu na maduka ya kuuza dawa. Shule, vituo vya kufanyia mazoezi, makumbusho, maeneo ya burudani na maeneo yalikuwa yamefungwa.
Jumamosi, Uhispania ambayo imerekodi maambukizi 7,753, na Ufaransa ambayo imeripoti visa 5,400 zilichukua hatua za dharura.
Serikali ya Uhispania imepiga marufuku watu kundoka majumbani isipokuwa tu kama wanaenda kununua vifaa muhimu kama vile dawa au kwenda kazini pekee.
Haki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Eneo karibu na Arc de Triomphe mjini Paris lilikuwa bila watu siku ya Jumapili
Ufaansa, migahawa, majumba ya sinema na maduka mengi yamefungwa.
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ametoa wito kwa nchi wanachama kukabiliana na janga la Corona kwa kuchukua hatua za dharura na kushirikiana.
Rais huyo amesema kuwa Muungano huo utaimarisha uzalishaji wa vifaa kama vile mashine za kuingiza hewa safi, barakoa, vifaa vya kufanyia majaribio virusi hivyo, na kugawanywa kwa nchi mbalimbali za Muungano wa Ulaya badala ya kila nchi kutengeneza vifaa vyake peke yake.
Uagizaji wa bidhaa hizo kwa nchi ambazo sio wanachama wa Muungano wa Ulaya utadhibitiwa kwa kiasi kikubwa.
Nini kinafanyika Coronavirus inapoingia mwilini?
Je juhudi za kutafuta chanjo ya coronavirus zimefika wapi?
Jinsi coronavirus inavyoisaidia filamu ya zamani kutazamwa sasa
Je nchi zingine duniani zinakabialiana vipi na virusi vya Corona?
Hadi kufikia sasa inakadiriwa kuwa watu 162,687 wameambukizwa virusi vya corona kote duniani huku chini tu ya idadi hiyo ikiwa ni kutoka China ambayo imerekodi visa 81,003. Inakisiwa kuwa watu 6,065 wamekufa, huku 3,085 wakiwa ni kutoka China.
Afrika Kusini inafunga mipaka yake kuanzia Jumatano kwa raia wa nje wanaotoka nchi ambazo zimeathirika vibaya na coronavirus.
Afrika Kusini ikiwa imerekodi visa 61, Rais Cyril Ramaphosa alisema kwamba nchi yake kwasasa inakabiliana na namna ya kusitisha virusi hivyo kusambaa na kuutangaza ugonjwa huo kama janga la taifa.
Marekani imepunguza ushuru wake hadi karibia sufuri kwa maslahi ya uchumi wake ambao unaendelea kudorora vibaya tangu janga la corona lililopotokea.
Ramani ya Coronavirus: Kasi ya kusambaa kwa virusi 16 Machi 2020
Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.
Sogeza uone ramani
Jumla ya visa vilivyothibitishwa Jumla ya vifo
168,134 6,480
Visa Vifo
Uchina 81,079 3,218
Italia 24,747 1,809
Iran 13,938 724
Korea Kusini 8,232 75
Uhispania 7,844 292
Ujerumani 5,795 11
France 4,500 91
Marekani 3,570 68
Uswizi 2,200 14
Uingereza 1,391 35
Norway 1,256 3
Netherlands 1,136 20
Sweden 1,032 3
Belgium. 886 4
Denmark 864 2
Austria 860 1
Japan 839 22
Mili ya Diamond Princess 696 7
Malaysia 428
Qatar 401
Ugiriki 331 4
Australia 297 3
Jamuhuri ya Czech 253
Israel 251
Canada 250 1
Ureno 245
Finland 244
Singapore 226
Slovenia 219 1
Bahrain. 214
Iceland 171 5
Estonia 171
Brazil 162
Ufilipino 140 12
Romania 139
Ireland 129 2
Poland 125 3
Saudi Arabia 118
Indonesia 117 5
Iraq 116 10
Thailand 114 1
India 113 2
Kuwait. 112
Misri 110 2
San Marino 109 7
Lebanon. 99 3
Milki za Kiarab 98
Luxembourg 77 1
Chile 74
Peru 71
Urusi 63
Afrika Kusini 61
Slovakia 61
Taipei ya China 59 1
Vietnam 56
Kashmir inayotawaliwa na Pakistan
53
Bulgeria 51 2
Brunei Darussalam 50
Croatia 49
Serbia 48
Algeria. 48 4
Argentina 45 2
Panama 43 1
Mexico 43
lbania 42 1
Colombia 34
Georgia 33
Hungary 32 1
Latvia 30
Morocco 28 1
Ecuador 28 2
Costa Rica 27
Belarus 27
Cyprus 26
Armenia 26
Senegal 24
Bosnia na Herzegovina 24
Moldova 23
Azerbaijan 23 1
Oman 22
Malta 21
Tunisia 20
Uturuki 18
Sri Lanka 18
Venezuela 17
Afghanistan 16
Macedonia Kaskazini 14
Maldivers 13
Lithuania 12
Jordan 12
Visiwa vya Faroe 11
Jamuhuri ya Dominica 11
Martinique 10
Jamaica. 10
Bolivia 10
Kazakhstan 9
New Zealand 8
Kisiwa cha Reunion 7
Paraguay 7
Cambodia 7
Guiana ya Ufaransa 7
Ghana 6
Rwanda 5
Puerto Rico 5
Jersey 5
Bangaldesha 5
Uruguay 4
Liechtenstein 4
Guyana 4 1
Cuba 4
Ukrain 3 1
Ushelisheli 3
Polynesia ya Ufaransa 3
Kenya 3
Honduras 3
Guadeloupe 3
Burkina Faso 3
Trinidad and Tobago 2 2
Nigeria 2
Namibia 2
Monaco 2
Saint Martin (Eneo la Ufaransa) 2
Saint Lucia 2
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo 2
Cameroon 2
Aruba 2
St St Vincent na Gradines 1
Vatican 1
Uzbekistan 1
Togo 1
Swaziland 1
Suriname 1
Sudan 1 1
Nepal 1
Mauritania 1
Mongolia 1
Guatemala 1
Equitorial Guinea 1
Guinea 1
Gibraltar 1
Guernsey 1
Gabon 1
Ethiopia 1
Visiwa vya Cayman 1
Congo 1
Cote d'voire 1
Jamuhuri ya Afrika ya Kati 1
Bhutan 1
Saint Barthéle. 1
Antigua na Barbuda 1
Andorra 1
Onesha kidogo
Chanzo: Chuo kikuu cha Johns Hopkins (Baltimore, Marekani), maafisa wa eneo
Mara ya mwisho kufanyiwa mabadiliko 16 Machi 2020, 04:00 GMT +1.
Uamuzi wa Marekani a kukagua raia wake wanaorejea nchini humo kutoka Uaya umesababisha ghasia katika viwanja vya ndege.
Utawala wa Trump umepiga marufuku raia wasio wa Marekani kutembelea nchi 26 za Muungano wa Ulaya na marufuku hiyo inatarajiwa kujumuisha Uingereza na Jamuhuri ya Ireland kuanzia Jumanne.
Marekani imerekodi vifo 62 vyenye kuhusishwa na coronavirus na maambukizi and 3,244.
Commentaires