Anza biashara yako kwa mtaji mdogo
Nimekuwa nikipokea maoni mengi sana kutoka kwa wasomaji wakitaka ushauri kuhusu biashara gani wanaweza kufanya kwa mtaji kidogo walioko nao. Huenda na wewe umeshajikuta kwenye njia panda kama hii na kushindwa kujua ufanye nini. Leo utajua ni kipi cha kufanya katika hali kama hii. Kabla ya kuendelea hebu tuone baadhi ya maoni ya wasomaji wenzetu waliotuandikia; Nimemalza chuo mwaka jana sijaajiriwa, nina ndoto za kujiajiri lakini mpaka sasa nmefanifakiwa kupata lak 3 so sjui nianzie wapi na nianze na lipi kwa huu mtaj maana kukodi frem tu ni elf 30/mwez na wanahtaj miez 6 Nahitaji kufanya biashara, na nimeshaanda mtaji kiasi kama cha millioni 2 . Tatizo langu nashindwa nifanye biashara gani na nianze vp? Naomba msaada wako. Ni mradi, miradi gani nianzise kwa mtaji wa laki mbili? Hayo ni baadhi tu ya maoni mengi ambayo nimepokea kuhusu changamoto ya biashara gani ya kufanya hasa mtu anapokuwa na mtaji kidogo. Kitu kikubwa ambacho mpaka sasa nimejifunza kutokana na mawasialiano na w...
Commentaires