MAISHA YANGU YA MAPENZI





Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tulikuwa tunapendana naye sana
Mpaka ilipo fikia tukawa tunapanga jinsi gani tunaweza kuowana kwa matatizo fulani ambayo alijitokezaga nyumbani kwetu yaani mama alikuwa amesha anza kuniambia nimesha kuwa inabidi Wapewe mahali zangu sasa yaani ikawa kama usumbufu nyumbani kila kukicha naambiwa vitu kama ivo mpaka nikawa naona kama imesha kuwa kero kwangu
Mpaka nikamwambia mpenzi wangu ambaye nilikuwa nampenda sana matatizo yaliopo nyumbani kwetu
Nilipo mwambiaga alinijibu kuwa yuko tayari kuniowa ila sio mali cash nikaona mpaka apo sio vibaya kama nitakuwa nawatokea wazazi wangu machoni itakuwa vyema zaidiili zile kelele za kila siku zinipungukie
Kufika juma tatu akaniambia Twende sokoni nikununulie nguo ambazo unapenda ili zikutaniwe home kwetu maana tulikuwa tunapanga kurendezana siku ya tatu
Tukaenda sokoni nikachagua nguo nyingi kweli nilipo rudi nyumbani nikawa napanga nguo zangu ambazo nitaenda nazo na zile ambazo nilikuwa napanga kuacha nikawa nawapa marafiki zangu kwasababu sikuwa na mdogo ata moja mwetu tulizaliwa wawili tu na dada yangu na amesha olewa kitambo
Ilipofika siku ya pili jioni akafika rafiki yangu nyumbani nakuniambia kwamba MAURIDI amerendeza nimeacha kwao kuko full vigere gere akika AIMERERANCE alikuwa ananiambia ivo nilikuwa sipo tena
Nilianguka gafla nikajikuta nimesha kuwa ospitalini nikawa najiuliza mengi ivi ni kweli Mauridi anaweza kunifanyia mimi kitu kama hichi nilikaaa siamini ila
Nilikubali baada yakuona nimekaa ospitali siku mbili bila kumuona akija kuniangalia
Nilipo rusiwa kurudi nyumbani nienda kwa dada maani sikujiskia ata kurudi nyumbani kwetu tena kwa kuepuka zile fujo za wazazi wangu
Mpaka sasa naishi sijuwi thamani ya kuwa na mpenzi maishani na sina ndoto yakuwa na mpenzi tena maishani mwangu.
Nawaombeni nyinyi mlie kwenye ndoa zitihini ndoa zenu msije kuzichezea siku moja maana ninavyo yajuwa maumivu ya mapenzi ni zaidi ya kifo
Mungu awabariki amen

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

Anza biashara yako kwa mtaji mdogo

Mambo 10 ambayo kijana hutakiwi kuyafanya

Jinsi ngono inavyo angamiza maisha ya vijana