Usikimbilie Kujenga Kabla Hujawa Na Uhakika Wa Kipato.
Karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa. Mpaka sasa tumeshajadili changamoto nyingi na kujifunza kupitia changamoto za wengine bonyeza hayo maandishi. Katika moja ya changamoto ambazo tumewahi kujadili ni kuhusu kujenga au kutokujenga hasa pale ambapo mtu anakuwa hana kipato cha uhakika. Katika makala; USHAURI; Kipi bora kujenga au kuwekeza kwenye biashara ? Tulijadili kwa kina kuhusu kipi bora kati ya kujenga au kuwekeza fedha hiyo kwenye biashara. Hivi karibuni msomaji mwenzetu ametupa maoni yake akieleza changamoto ambayo inamkabili. Changamoto hii ni sawa kabisa na ile tuliyojadili ya kuhusu kujenga au kuwekeza kwenye biashara, ila changamoto yake imeenda mbali kidogo hivyo nimeona ni bora tuijadili tena. Kabla hatujaingia kwenye ushauri naomba nikupe nafasi ya kusoma kile ambacho tumeandikiwa na msomaji mwenzetu; Ndugu yetu huyu ameuliza maswali mawili ya muhimu sana kwake yanayompatia ...